NJIA RAHISI YA WOKOVU WA MUNGU
Rafiki yangu:Ninakuuliza
swali muhimu maishani mwako. Furaha yako ya milele au huzuni yako ya
milele inategemea jibu Ia swali hili. Swali ni hili:Je,
umeokolewa?Si swali la jinsi
ulivyo mwema, wala si swali la kama u mshiriki wa kanisa, bali:Je,
umeokolewa? Una uhakika kwamba utaenda mbinguni utakapokufa?
Mungu anasema kwamba, ili uende
mbinguni, ni lazima uzaliwe mara ya pili. Katika Yohana 3:7, Yesu
alisema kwa Nikodemo,
“Ni lazima
uzaliwe mara ya pili.”
Katika Biblia Mungu anatupatia njia ya
pekee ya kuzaliwa mara ya pili, yaani kuokolewa.Njia yake ni rahisi!
Unaweza kuokolewa leo. Vipi?
Kwanza, rafiki yangu, ni lazima
utambue kwambawewe u mwenye
dhambi.“Kwa sababu wote wamefanya
dhambi,na kupungukiwa na utukufu
wa Mungu”(Warumi 3:23).
Kwa sababu u mwenye dhambi,umehukumiwa
kufa.“Kwa maana mshahara wa
dhambi ni mauti”(Warumi 6:23). Hii
ina maana kutengwa na Mungu katika jehanum milele.“Na
kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa
hukumu”(Waebrania 9:27).
Lakini Mungu alikupenda mno hata
akamtoa Mwanawe pekee, Yesu,
ili azichukue dhambi zako na kufa pahali pako.“Yeye
asiyejua dhambi[Yesu, ambaye
hakujua dhambi yo yote]alimfanya
kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu
katika Yeye”(2 Wakorintho 5:21).
Ilimbidi Yesu amwage damu yake na
kufa.“Kwa kuwa uhai wa mwili u
katika hiyo damu”(Mambo ya Walawi
17:11).“. . . Pasipo kumwaga damu
hakuna ondoleo[msamaha]”(Waebrania
9:22).
“Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye
mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu,
tulipokuwa tungali wenye dhambi”(Warumi
5:8).
Ingawa hatuelewi ni jinsi gani, Mungu
alisema kuwa dhambi zangu na dhambi zako ziliwekwa juu ya Yesu naalikufa
pahali petu.Yesu akawafidia
yetu[badala yetu].Ni kweli.
Mungu hawezi kusema uongo.
Rafiki yangu,“Mungu
. . . anawaagiza watu wote wa kila mahali watubu”(Matendo
17:30). Kutubu huku au toba hii ni badiliko la nia akilini;
kukubaliana na Mungu kuwa mtu ni mwenye dhambi, na kukubaliana na
yale aliyoyafanya Yesu kwa ajili yetu msalabani.
Katika Matendo 16:30-31, mlinzi wa
gereza wa Filipi aliwauliza Paulo na Sila,“Mabwana,
yanipasa nifanye nini nipatekuokoka?Wakamwambia,mwaminiBwana
Yesu, nawe utaokoka . . . .”
Mwamini tu Bwana Yesu ambaye alibeba
dhambi zako, akafa badala yako, akazikwa, na Mungu alimfufua.Ufufuo
wake unahakikisha kwa nguvukuwa
aaminiye anaweza kudai uzima wa milele anapompokea Yesu kuwa Mwokozi
wake.
“Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa
kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake”(Yohana
1:12).
“Kwa kuwakilaatakayeliitia
jina la Bwanaataokoka”(Warumi
10:13). Neno“kila”linakujumlisha
na wewe.“Ataokoka,”
maana yake si labda, au inawezekana, bali
ni kwa uhakika“ataokoka.”
Hakika, unatambua kuwa u mwenye dhambi?
Po pote ulipo sasa hivi, ukitubu, inua moyo wako kwa Mungu katika
maombi.
Katika Luka 18:13, mwenye dhambi mmoja
aliomba:“Ee Mungu, uniwie radhimimi
mwenye dhambi.”Basi
omba:“Ee Mungu, ninajua kuwa
ni mwenye dhambi. Ninaamini kuwa Yesu alikuwa fidia yangu alipokufa
msalabani. Ninaamini damu yake aliyomwaga, kufa kwake, kuzikwa kwake,
na kufufuka kwake kulikuwa kwa ajili yangu. Sasa ninampokea awe
Mwokozi wangu. Asante kwa msamaha wa dhambi zangu, zawadi ya wokovu
na uzima wa milele, kwa sababu ya neema yako ya huruma. Amina.”
Mwamini Mungu katika Neno lake, na dai
wokovu wake kwa imani. Amini, na utaokoka. Hakuna kanisa, wala jumba,
wala matendo mema yawezayo kukuokoa.Kumbuka,
Mungu ndiye aokoaye. Basi!
Njia rahisi ya wokovu ya Mungu ni:Wewe
u mwenye dhambi na usipomwamini Yesu ambaye alikufa pahali pako,
utakaa milele jehanum. Ukimwamini kuwa Mwokozi wako ambaye
alisulubiwa, akazikwa, akafufuka, utapokea msamaha wa dhambi zako
zote, na utapokea zawadi [karama] ya uzima wa milele kwa imani.
Unasema, “Kweli, haiwezi kuwa rahisi
hivi.”Ndiyo, ni rahisi hivyo! Ndivyo ulivyo mpango wa Mungu wa
wokovu katika Maandiko.Rafiki
yangu, mwamini Yesu na kumpokea kuwa Mwokozi wako leo.
Ikiwa huu mpango wake wa wokovu hauko
wazi au haueleweki kwako, soma kijikaratasi hiki tena na tena,
pasipo kukiweka chini, mpaka umeuelewa ujumbe wake. Nafsi yako ni ya
thamani zaidi kuliko vyote vya ulimwengu.
“Kwa kuwa itamfaidia mtu nini kuupata
ulimwengu wote, akipata hasara ya nafsi yake?”(Marko
8:36).
Hakikisha kwamba umeokoka. Ukipoteza
nafsi yako utapoteza mbingu na utapoteza vyote. Tafadhali, mruhusu
Mungu akuokoe sasa hivi.
Nguvu ya Mungu itakuokoa, itakulinda,
na kukuwezesha kuishi maisha ya ushindi ya Kikristo.“Jaribu
halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu; ila Mungu
ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini
pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze
kustahimili”(1 Wakorintho 10:13).
Usitegemee hisia zako – jinsi
unavyojisikia. Hisia zinabadilika-badilika. Simama juu ya ahadi za
Mungu. Ahadi za Mungu hazibadiliki. Ukiisha kuokoka, kuna mambo
matatu ya kufanya kila siku ili ukue kiroho:Omba–
unazungumza na Mungu.Soma
Biblia yako– Mungu anazungumza
nawe.Shuhudia–
waambie watu wengine kwa niaba ya Mungu.
Unapaswa kubatizwa katika utii kwa
Bwana Yesu Kristo kuwa ushuhuda wa hadhara wa wokovu wako, halafu,
bila kuchelewa, jiunge na kanisa ambalo linaamini Biblia.“Basi
usiuonee haya ushuhuda wa Bwana wetu . . . ”(2
Timotheo 1:8).
“Basi, kila mtu atakayenikiri mbele ya
watu, nami nitamkiri mbele za Baba yangu aliye mbinguni”(Mathayo
10:32).
|